Email: info@jkuz.go.tz | P.o.Box: 985 | Tel: 0242238030 | Fax: 0242232149
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ndugu Ali Abdul-ghulam Hussein amezipongeza Skuli za Ufundi na Sekondari JKU Mtoni kwa jitihada za kuimarisha Sekta ya Elimu Nchini
Ameyasema hayo katika Ukumbi wa Skuli ya U JKU wakati wa mahafali ya kuwapongeza wanafunzi wa Skuli za Ufundi na Sekondari JKU Mtoni
Amesema ni jukumu la wazazi na walezi kuwekeza elimu kwa watoto wao ili waweze kupata fursa za kuendelea na elimu ya juu sambamba na kupata nafasi za kimasomo ndani na nje ya Nchi ili kuweza kujikwamua katika maisha yao ya badae
Hata hivyo ameahidi kuwapatia walimu wa Skuli ya Sekondari vishkwambi kwa lengo la kuwaongezea uwezo sambamba na kuendana na wakati katika ufundishaji
Nae Mkuu wa JKU Kanali Makame Abadalla Daima amesema mafanikio ya Skuli za Ufundi na Sekondari JKU Mtoni yanatokana na mashirikiano baina ya wazazi, wanafunzi pamoja na jitihada zinazofanywa na walimu hasa katika kudumisha nidhamu katika kipindi chote cha masomo
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Skuli za Ufundi na Sekondari Kanali Jabir Saleh Simba amesema jumla wanafunzi 234 wamefanya mitihani ya kidatu cha nne na wote wamefanikiwa kufaulu katika daraja la kwanza la pili na la tatu jambo ambalo limeiyongezea sifa Skuli ya JKU
Akisoma taarifa kwa niaba ya wanafunzi wenzake Talatham Abadalla Mussa amesema licha ya ufaulu mzuri uliopatikana likini kuna changamoto ndogo ndogo kama vile ukosefu wa usafiri pamoja na dahalia ambalo lingesaidia wanafunzi katika jitihada za masomo
MKUTANO MKUU WA JKU WA MWAKA 2022-2023
WAHITIMU WA KOZI YA UONGOZI MDOGO INT 018/2023 JKU DUNGA KUONYESHA UKOMAVU WAO KATIAK MAFUNZO