Email: info@jkuz.go.tz | P.o.Box: 985 | Tel: 0242238030 | Fax: 0242232149
Mkuu wa Utawala Wa JKU Kanali Haji Ali Ali amempongeza Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pamoja na uongozi wa Halmashauri ya Magharibi B kwa kuliamini Jeshi la Kujenga Uchumi katika ujenzi wa miradi mbalimbali
Ameyasema hayo wakati akikabidhi mradi wa ujenzi wa milango ya maduka ya wajasiriamali iliopo katika maeneo ya Kwa Mchina Wilaya ya Magahribi “B’ Unguja
Amesema kukamilika kwa mradi huo kunatokana na juhudi kubwa zilizofanywa na wana JKU pmoja na kuwatumia ipasavyo vijana wa Ujenzi wa Taifa jambo ambalo limepelekea kukamilika kwa wakati na ubora unaokubalika
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B’ Bi Hamida Musa Khamis amesema kua kukamilika kwa jengo hilo kutawasaidia wajasria mali kufanya biashara katika maeneo maalum yaliotengwa na Serekali jambo ambalo litaongeza usafi wa mazingira hasa katika walaya hio
Aidha amefafanua kua zaidi ya shilingi bilioni moja zimetumika katika mradi huo ambapo linatarajiwa kuendelezwa na kufikia milango 96 ambayo watapatiwa wajasiriamali mbalimbali wa wilaya hio
Kwa upande wake mmoja wa wajasiriamali waliopata nafasi katika maeneo hayo Bi Asha Suleiman Saidi ameushkuru uongozi wa Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwapatia maduka hayo na kuahidi kuyafanyia kazi iliokusudiwa sambamba na kuyatunza ili iweze kudumu kwa muda mrefu
MKUTANO MKUU WA JKU WA MWAKA 2022-2023
WAHITIMU WA KOZI YA UONGOZI MDOGO INT 018/2023 JKU DUNGA KUONYESHA UKOMAVU WAO KATIAK MAFUNZO