Email: info@jkuz.go.tz | P.o.Box: 985 | Tel: 0242238030 | Fax: 0242232149
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar Kanali Makame Abdalla Daima amewataka Wanafunzi Askari wa Kozi ya Uongozi Mdogo kuzingatia mafunzo watakayopatiwa ili kuwajengea uwezo katika majukumu yao ya kila siku.
Ameyasema hayo wakati alipofungua kozi ya uongozi hapo katika Chuo cha Uongozi JKU Dunga Wilaya ya Kati Unguja.
Amesema mafunzo hayo yatawasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza ufanisi wa kazi zao sambamba na kuleta maendeleo ya ndani ya JKU na Taifa kwa ujumla.
Aidha amewataka askari hao kuchunga nidhamu, uadilifu na utiifu ili kuweza kufanikisha malengo makuu ya hafunzo hayo.
Nae mkuu wa idara ya mafunzo na utendaji kivita Meja Khamis Juma amesema jumla ya wanafunzi 242 kutoka kambi mbalimbali za Unguja na Pemba watapatiwa mafunzo mbalimbali kama vile Mbinu za kivita, Ujanja wa porini, Uomaji wa ramani, Usalama na utambuzi pamoja na somo la uzalendo.
JKU YAFANYA KAZI USIKU NA MCHANA KATIKA UJENZI WA MRADI WA SOKO LA MWANAKWEREKWE
MKUU WA WILAYA YA MJINI AKABIDHIWA MRADI WA MAJENGO YA WAJASIRIAMALI NA JESHI LA KUJENGA UCHUMI