Email: info@jkuz.go.tz | P.o.Box: 985 | Tel: 0242238030 | Fax: 0242232149
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Uchumi JKU Kanali Makame Abdalla Daima aliwataka wahitimu wa kozi ya Uongozi wa kati kuyatumia vyema mafunzo waliyopata kwa lengo la kuongeza ufanisi ndani ya jeshi hilo.
Aliyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya kozi ya uongozi wa kati mkupuo wa 08 \2022 iliyofanyika katika Chuo cha uongozi JKU Dunga Wilaya ya Kati Unguja .
Alisema kuwa madhumuni makuu ya mafunzo hayo ya kijeshi ni kuwajengea uwezo wa kiutendaji watumishi wa JKU sambamba na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku
Hata hiyo alieleza kuwa nidhamu , uwajibikaji na ushirikiano katika kazi ndio njia pekee itakayosaidia kuongeza uzalishaji katika kambi mbalimbali za JKU.
Akisoma taarifa ya mkufunzi mkuu wa kozi hiyo Luteni Idi Haji Makame alisema kuwa jumla ya wanafunzi 427 wamefanikiwa kuhitimu mafunzo ya miezi minne [4] katika masomo mbalimbali ya kijeshi kama vile Ujanja wa porini Usomaji wa ramani, Mbinu za kuvita pamojana uzalendo wanchi yao .
Akisoma taarifa kwa niaba ya wahitimu wenzake mteule daraja la pili Nasra Abdala Makolela alisema kuwa licha ya mafanikio waliyoyapata lakini pia kuna changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na udongo wa kituo cha afya na ukosefu wa vifaa tiba, ukosefu wa maktaba ya kijeshi pamoja na uchakavu wa miundombinu ya barabara .
Hata hivyo alieleza kuwa pamoja kushiriki kikamilifu katika mafunzo hayo pia walishiriki katika majukumu mbali mbali ya Kitaifa kama vile zoezi la Linda Kisiwa namba mbili ( 2 ) pamoja na kushiriki katika Sensa ya Watu na Makaazi
Alisema mbali na mafunzo hayo lakini pia wamefanikiwa kuchangia jumla ya shilingi milioni arubaini na sita laki tisa na elfu sabiini ambazo zitasaidia katika ujenzi wa ofisi , vyoo, pamoja na mnara wa maji ili kuweka alama ndani ya chuo hicho .
Sherehe hizo ziliambatana na utoaji wa vyeti na zawadi kwa wanafunzi walofanya vizuri pomoja na maonyesho ya harusi za kijeshi , kwata ya kitara pamoja na kwata ya kutawanya mikusanyiko haramu.
JKU YAFANYA KAZI USIKU NA MCHANA KATIKA UJENZI WA MRADI WA SOKO LA MWANAKWEREKWE
MKUU WA WILAYA YA MJINI AKABIDHIWA MRADI WA MAJENGO YA WAJASIRIAMALI NA JESHI LA KUJENGA UCHUMI