Email: info@jkuz.go.tz | P.o.Box: 985 | Tel: 0242238030 | Fax: 0242232149
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar Kanali Makame Abdalla Daima amewataka wapiganaji wa JKU kuongeza bidii katika uzalishaji wa mazao ya chakula na mbogamboga ili kukuza kipato ndani ya Jeshi hilo.
Ameyasema hayo wakati akizindua uvunaji wa zao la viazi vitamu na kebege (kabich) uliofanyika katika Kikosi cha JKU Bambi Matola Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema kutokana na mahitaji makubwa ya mazao ya chakula na mbogamboga visiwani Zanzibar , JKU ipo katika mkakati maalumu wa kuimarisha kilimo cha aina mbalimbali ili kupunguza uagizaji wa bidhaa za chakula kutoka nje ya nchi.
Kwa upande wake mkuu wa Kikosi cha JKU Bambi Matola Kapteni Suleiman Benjamin Simon amesema kua jumla ya ekari ishirini na saba (27) za viazi vitamu na kebich zimelimwa kikosini hapo ambazo zitasaidia kwa kiasikikubwa kuongeza kipato ndani ya JKU pamoja na upatikanaji wa chakula kwa askari na vijana wa ujenzi wa Taifa.
JKU YAFANYA KAZI USIKU NA MCHANA KATIKA UJENZI WA MRADI WA SOKO LA MWANAKWEREKWE
MKUU WA WILAYA YA MJINI AKABIDHIWA MRADI WA MAJENGO YA WAJASIRIAMALI NA JESHI LA KUJENGA UCHUMI