Email: info@jkuz.go.tz | P.o.Box: 985 | Tel: 0242238030 | Fax: 0242232149
Katika mfumo wa uongozi Kamanda Mkuu wa JKU ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi [Sheria namba 6 ya mwaka 2003, kifungu 6 (1)]. Kutokana na mfumo huo JKU inakuwa chini ya Wizara ya Nchi afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ ambayo huongozwa na Waziri husika wa Wizara hiyo. Katika Uongozi wa JKU wenyewe, Mkuu wa JKU anakuwa Mkuu wa Jeshi akisaidiwa na Mkuu wa Utawala ambae ndie Mtendaji Mkuu wa Majukumu ya kila siku. Kufatana na mfumo huu wa kiutendaji muundo wa JKU unakuwa kama ifuatavyo:- Kamanda Mkuu wa JKU (Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Waziri wa Wizara ya Nchi (OR) Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ
Mkuu wa JKU Kanali Daima Amewataka Maafisa na Wapiganaji Kuzidisha Mazoezi ili kulinda Afya zao
JKU Yaimarisha Huduma za Kinywa na Meno Katika Hospitali ya Makao Makuu ya JKU Saateni.
Mkuu wa JKU Awaongoza Maafisa na Wapiganaji pamoja na Vijana wa Kujenga Taifa katika mazoezi.