Email: info@jkuz.go.tz | P.o.Box: 985 | Tel: 0242238030 | Fax: 0242232149
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Uchumi Kanali Makame Abdalla Daima amewataka wanafunzi wa Chuo cha Uongozi JKU Dunga kuzingatia Mafunzo wanayopatiwa ili kuongeza ufanisi wa kazi zao. Ameyasema hayo wakati akifungua Mafunzo ya Uongozi wa kati Mkupuo wa 8/2022 uliofanyika katika Chuo cha Uongozi JKU Dunga Wilaya ya Kati Unguja. Amesema dhamira ya mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo na ufahamu wa majukumu yao ili kupeleka mbele maendeleo ya JKU na Taifa kwa Ujumla. Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mafunzo na Utendaji Kivita Meja Jafar Khamis Juma amesema kuwa jumla ya askari 429 wanatarajiwa kupata mafunzo mbali mbali yakiwemo Usalama na Utambuzi, Mbinu za kivita, Ujanja wa Porini, Huduma ya Kwanza pamoja na Uzalendo ambayo yatachukua muda wa Miezi Minne.
SENSA KUHESABIWA JKU DIAMOND KWAYA
Mhe. Rais wa Zanzibar atembelea mabanda ya J K U katika Maonesho Ya siku ya Wakulima Duniani.