Email: info@jkuz.go.tz  |  P.o.Box: 985  |  Tel: 0242238030  |  Fax: 0242232149


Logo
HABARI NA MATUKI0

Ziara ya Waziri wa Nchi OR-TMSMIM katika skuli za JKU mtoni

Created at 1 year ago

Mkuu wa JKUZ

Walimu wa skuli ya ufundi jku mtoni wameomba kuandaliwa utaratibu wa kupatiwa stahiki za mafao yanayoendana na mazingira ya kazi yao, kwani itawaongezea moyo wa kujituma zaidi katika kuwapatia vijana taaluma muhimu kwa maisha yao ya baadae.

Wakizungumza na waziri wa nchi afisi ya rais tawala za mikoa serikali za mitaa na idara maalum za smz, mh masoud ali mohamed alipotembelea skuli hiyo, walimu hao wamesema wamekuwa na jitihada za kuhakikisha kuwa taaluma inayotolewa inawanufaisha idadi kubwa ya vijana, na kulijengea sifa jeshi hilo kutokana na ufanisi unaopatikana.

Aidha wameomba kupatiwa vifaa kwa ajili mafunzo ya vitendo ili kuwajengea uwezo wa kufahamu vyema taaluma  wanayopatiwa katika fani mbali mbali.

Akizungumza na uongozi pamoja na walimu wa skuli hiyo mh. Masoud amesema skuli nyingi zimeshindwa kufikia malengo waliyojipangia kutokana na kukosekana kwa nidhamu na uadilifu wakati wa utekelezaji wa majukumu yao, hivyo ameutaka uongozi kuhakikisha unasimamia utaratibu wa kuwapatia stahiki watendaji hao.

 

 

  

 

 

SENSA KUHESABIWA JKU DIAMOND KWAYA

Mhe. Rais wa Zanzibar atembelea mabanda ya J K U katika Maonesho Ya siku ya Wakulima Duniani.


WASILIANA NASI
  • Email: info@jkuz.go.tz
  • P.O.Box: 985
  • Fax: 0242232149
  • Tel: 0242238030
WALIOTEMBELEA TOVUTI